Posts

Showing posts from March, 2022

Nagaga yetu

Nagaga ni mji mdogo unaopatikana wilaya ya masasi. Nagaga ni miongoni mwa miji inayokua kwa kasi katika wilaya hii ya masasi. Miongoni mwa vitu vinavyoufanya mji wa nagaga ukue kwa kasi ni upatikanaji wa huduma za kijamii. Katika mji wa nagaga kuna kituo kikubwa cha afya ambacho kinategemewa na sehehemu kubwa ya watu wanaopatikana jimbo la lulindi. huduma zote muhimu za kiafya zinatolewa katika kituo cha afya nagaga ikiwemo upasuaji mdogo, uongezewaji wa damu na vipimo vya magonjwa mbalimbali. Pia katika mja wa nagaga kuna shule ya msingi, pia sekundari ya kutwa inayopatikana takriban umbali wa kilmita moja kutoka narabara kuu. Nagaga kuna huduma ya maji yanayopatikana kwa uhakika katika msimu wote wa mwaka. Pia huduma ya umeme ni ya uhakika katika mji wa nagaga. Mji wa nagaga umekuwa maarufu zaidi kutokana na muingiliano mkubwa wa watu hivyo umekuwa ni mji muhimu katika biashara. wastani wa muingiliano wa wageni kwa siku ni watu mia tano hadi elfu tano. Karibuni sana nagaga

Habarini wakuu.

Karibuni sana kwa habari mbalimbali, Tangaza nasi